Mlinzi kiraka wa Yanga Ally Mtoni 'Sonso' amewaomba radhi mashabiki na wadau wa soka nchini kufuatia tukio lisilo la kiungwana alilofanya kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc na kupelekea akatolewa nje kwa kadi nyekundu
Mtoni pia amewaomba radhi wachezaji na viongozi wa Yanga, Azam Fc na TFF kufuatia tukio hilo
"Naomba msamaha kwa wana michezo wote kwa kadi niliyoipata siku ya jana kutokana na tukio nililofanya kwenye mchezo wetu vs Azam fc," amesema Mtoni
"Kweli mchezo wa mpira ni mchezo wa furaha na upendo kwa kuwa ni ajira ila changamoto za hapa na pale zipo pia"
"Naomba msamaha kwa Wachezaji,viongozi wangu wa Yanga na pia hata wa Azam Fc na hata viongozi wenye dhamana na soka letu TFF na sitaweza kuja rudia tukio la aina ile"
ADVERTISE HERE