Yanga kurejea Dar leo, kuiwinda Prisons

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2020
Yanga kurejea Dar leo, kuiwinda Prisons

Jumapili ya Januari 26 2020 kwenye uwanja wa Uhuru, kikosi cha Yanga kitashuka dimbani kuikaribisha Tanzania Prisons katika mchezo wa raundi ya nne kombe la FA (ASFC)

Timu hizo zinakutana kwa mara ya pili msimu huu, Yanga ikishinda kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu uliozikutanisha timu hizo mkoani Iringa

Wakati kikosi cha Tanzania Prisons kikiwa hakina mabadiliko, hali itakuwa tofauti kwa Yanga iliyosukwa upya katika usajili wa dirisha dogo

Wachezaji wapya saba wameongezwa Yanga huku wengine sita wakionyeshwa mlango wa kutokea

Maboresho hayo yameiongezea Yanga makali, sasa ikicheza kandanda la kushambulia muda mwingi tangu ujio wa kocha Luc Eymael

Yanga inatokea mkoani Singida ambako jana ilipata ushindi wa mabao 3-1 huku kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison aliyetua wiki iliyopita akiwaongezea makali mabingwa hao wa kihistoria

Baada ya kukosa taji lolote kwa misimu miwili, Yanga imedhamiria kuondoka na taji msimu huu hesabu kali zikipigwa kwa taji hili la FA na ligi kuu

Ushindi katika mchezo huo utawahakikishia kutinga hatua ya 16 bora mchezo mmoja kuelekea hatua ya robo fainali

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1m ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’