Mashine zote ziko fiti, watapona kweli?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2017
Mashine zote ziko fiti, watapona kweli?
Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Donald Ngoma wameungana na kikosi cha Yanga kilicho 'mafichoni' kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba Jumamosi.

Wachezaji hao wote waliachwa katika safari ya Yanga kanda ya ziwa kwenye michezo ya VPL dhidi ya Kagera Sugar na Stand United.

Kamusoko alikuwa akisumbuliwa na majeraha ya kisigino huku Ngoma akisumbuliwa na matatizo ya misuli. Tambwe yeye alikuwa na tatizo la goti lililomuweka nje tangu mwanzoni mwa msimu.

Lakini sasa kulingana na Daktari wa Yanga, Dk Edward Bavu, wachezaji hao wote wako fiti na hata walipoachwa jijini Dar es salaam walikuwa wakifanya mazoezi ya nguvu.

Kurejea kwa wakali hao kunaongeza upana wa kikosi cha Yanga ambacho kimeshawasha 'engine' ya kuelekea kwenye ubingwa wa nne mfululizo.

Yanga imeweza kushinda michezo yake yote ya kanda ya ziwa licha ya kuwakosa wachezaji hao ambapo washambuliaji Obrey Chirwa na Ibrahim Ajib waliweza kutengeneza ushirikiano hatari uliopeleka hofu Msimbazi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’