Kikosi cha Yanga tayari kimerejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili Januari 26 kwenye uwanja wa Uhuru/Taifa
Yanga ilikuwa Singida ambako juzi ilifanikiw akuondoka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji wao Singida United katika mchezo wa ligi kuu
Mabingwa hao wa kihistoria wana siku mbili za kujiandaa na mtanange huo wa kukata na shoka ambao ushindi utawahakikishia kutinga raundi ya tano ambayo ni hatua ya 16 bora
Leo Yanga inatarajiwa kujifua kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii jijini Dar es salaam
ADVERTISE HERE