Zahera asifu mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Jan 2020
Zahera asifu mabadiliko Yanga

Aliyekuwa Mkufunzi wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu hiyo imeonyesha mabadiliko makubwa ya uchezaji juzi walipoikabili Singida United

Zahera ambaye yupo mbioni kujiunga na Buildcon ya Zambia, bado yuko nchini akiwa ameweka makazi yake ya muda

Ameeleza kuvutiwa na mbinu za Mbelgiji Luc Eymael ambapo amemtabiria kuwa ataweza kutengeneza timu ya ushindani

"Nimpongeze kocha kwa kuiwezesha Yanga kucheza mpira mzuri na wakuvutia tofauti na mchezo wao uliopita, naamini kama kocha atapewa nafasi ya kufanya kazi yake watakuwa na kikosi bora kwa misimu ijayo," amesema Zahera

"Binafsi sikushangaa matokeo yao ya awali walipofungwa na Kagera Sugar,  nilijua ni ugeni wa mbinu za kocha kwa wachezaji,  lakini kwa sababu wachezaji wengi nawajua nilikuwa na matumaini ya kubadilika kwa kikosi katika mechi zinazokuja, kocha anastahili pongezi hizi"

Aidha Mcongomani huyo amesifu usajili wa kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ambapo amesema mchezaji huyo atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

"Nimemuona mchezaji wao mpya waliomleta juzi (Morrison), ni mchezaji mzuri sana, Nadhani kama kocha ataweza kumtumia vizuri, atawasaidia"

"Mchezaji huyu akitumika vizuri pamoja na Molinga nadhani watafunga mabao mengi"

Zahera alitimuliwa Yanga baada ya timu kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kwa kipigo cha jumla cha mabao 5-1 kutoka kwa Pyramids ya Misri

Mcongoani huyo alisajili nyota wapya 12 kwenye kikosi chake, hata hivyo miongoni mwao, nyota watano wa kigeni wameachwa

Wachezaji aliowaleta mwezi Julai lakini tayari wameachwa ni Sadney Urikhob, Juma Balinya, Mustafa Selemani, Maybin Kalengo na Issa Bigirimana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’