Nyota wawili wa Yanga Ditram Nchimbi na Feisal Salum wanatarajiwa kuelekea nchini Misri kufanya majariboio kunako klabu ya Smouha inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo
Nyota hao huenda wakaondoka Januari 27 baada ya mchezo wa raundi ya nne michuano ya kombe la Azam kati ya Yanga dhidi ya Prisons ambao utapigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa
Inaelezwa kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael ndiye aliyezuia kuondoka kwa wachezaji hao mapema licha ya kuwa taratibu zao za safari zilikuwa zimekamilishwa
Wadau washangaa kuitwa kufanya majaribio
Baadhi ya wadau wameshangazwa na Yanga kukubali mpango wa Smouha kuwataka wachezaji hao kwa majaribio kwanza licha ya kuwa wanazo sifa za kusajiliwa bila ya kufanyiwa majaribio
"Wachezaji wote wamecheza timu ya Taifa kwa nyakati tofauti, Feisal alicheza mpaka michuano ya Afcon 2019, sio mchezaji wa kwenda kufanya majaribio, tena hapa Misri?"
"Mbona kuna nyota wengi wa Kitanzania wamesajiliwa huko Misri bila majaribio mfano Himid Mao, Yahya Zayd na hata Shiza Kichuya ambaye ameshindwa mwenyewe kupambana na kuamua kurudi Simba"
"Pia wapo akina Saimon Msuva ambao walisajiliwa moja kwa moja Morocco? Nadhani vilabu vinapaswa kuwapa thamani wachezaji wake, wakati mwingine sio kila mchezaji anapaswa kufanya majaribio hasa hapa Afrika"
"Baadhi ya vilabu vinatumia mbinu hii ili wawanunue kwa bei ndogo. Lakini pia ikumbukwe mchezaji akienda kufanya majaribio anaweza kuumia halafu timu ikaachana na mpango wa kumsajili, hasara inarudi kwenu," alisema Yusufu, Mdau wa Mwana Jangwani