Kila mchezaji ana nafasi Yanga - Eymael

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2020
Kila mchezaji ana nafasi Yanga - Eymael

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema kikosi chake kimesheheni wachezaji wenye vipaji na kuwa kila mchezaji atapata nafasi ya kucheza

Mbelgiji huyo amesema kwenye timu yake hakuna aliyejihakikishia namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza

Eymael alitoa kauli hiyo jana baada ya mchezo wa kombe la Azam kati ya Yanga dhidi ya Prisons ambao ulimalizika kwa ushindi wa mabao 2-0

Kwenye mchezo huo Mu Ivory Coast Yikpe Gnamien alipachika bao la pili wakati bao la kwanza likiwekwa kimiani na Bernard Morrison kwa mkwaju wa penati

Eymael alieleza kuvutiwa na Gnamien ambaye amefunga katika michezo miwili mfululizo akitokea benchi

"Yikpe ni mchezaji anayejituma, nafurahi anapoingia mara nyingi anafanya kile ninachomuelekeza. Anaingia kwenye mfumo taratibu, wakati ukifika ataanza kwenye kikosi cha kwanza," alisema Eymael

"Tuna wachezaji wengi wazuri, kila mchezaji ana nafasi kwenye timu yangu, muhimu ni kuhakikisha anajituma na kuonyesha ubora wake"

Baada ya ushindi wa kombe la FA, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Februari mosi kwenye uwanja wa Uhuru

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’