Ukizungumzia wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga sasa huwezi kukosa kutaja jina la kiungo mshambuliaji Deus Kaseke
Hakuwa akiaminiwa sana wakati wa Mwinyi Zahera, lakini tangu alipokuja Mkwasa na sasa Luc Eymael, amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga
Kaseke anaipa faida Yanga timu inaposhambulia lakini pia ana mchango mkubwa pale timu inapojilinda
Aidha ujio wa mafundi kina Haruna Niyonzima, Bernard Morrison na uwepo wa kina Mapinduzi Balama kwenye safu ya kiungo ni kama wamemrejesha misimu minne wakati huo akiwa kwenye kiwango cha juu
Kwa hakika furaha ya mataji inaweza kurejea msimu huu kama nyota hawa wataendeleza moto walionao sasa
ADVERTISE HERE