Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison ameeleza kufurahia mapokezi aliyopewa na mashabiki wa timu hiyo akiwa ndio kwanza ametimiza wiki mbili tangu ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria akitokea klabu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Morrison amesema mapokezi aliyopewa na mashabiki wa Yanga ni ya kushangaza, jambo linamuongezea ari ya kupambana ili kuwapa furaha
"Aina ya upendo ambao nimepata kutoka kwa watu wa Tanzania haswa mashabiki wa Yanga ni ya kushangaza, ulinikaribisha nyumbani kwako na mikono wazi, nakuahidi kufanya bidii yangu na kufanya bidii kutufanya wote tufurahi. Nawapenda nyote," aliandika Morrison kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
Morrison ameanza na rekodi za kutisha kwenye kikosi cha Yanga. Katika michezo miwili aliyotumika, amefunga bao moja na kutengeneza maba mengine matatu
Keshokutwa Jumapili anatarajiwa kuwaongoza mabingwa hao wa kihistoria kuwakabili Mtibwa Sugar katika mchezo mwingine wa ligi kuu