Eymael, Mkwasa 'kombinesheni' imekubali

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2020
Eymael, Mkwasa 'kombinesheni' imekubali

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael alianza majukumu yake vibaya kwenye kikosi cha Yanga akipoteza michezo yake yote miwili ya kwanza

Hali hiyo ilipelekea kuibuka kwa sintofahamu kwenye benchi la ufundi ambapo kwa nyakati tofauti ilielezwa Eymael alipendekeza aletewe kocha mwingine msaidizi badala ya Charles Mkwasa aliyekuwa pendekezo la uongozi wa Yanga

Hata hivyo sasa inaelezwa Eymael ameridhia kufanya kazi na Mkwasa baada ya kujiridhisha kuwa anahitaji uzoefu wa nguli huyo wa klabu ya Yanga

Kabla ya uamuzi huo, uongozi wa Yanga ulikuwa mbioni kumalizana na mkufunzi wa Kagera Sugar Meckie Mexime

Chini ya Eymael na Mkwasa, Yanga sasa imeshinda michezo mitatu mfululizo tangu walipopoteza michezo miwili ya kwanza

Jambo jema zaidi, kiwango cha mabingwa hao wa kihistoria kimeendelea kuimarika siku hadi siku jambo linalowapa furaha mashabiki

Mkwasa alikabidhiwa majukumu ya kuinoa Yanga kwa muda baada ya uongozi wa timu hiyo kuachana na aliyekuwa kocha mkuu, Mwinyi Zahera mwezi Novemba 2019

Yanga haikupoteza mchezo wowote katika kipindi chote ambacho ilikuwa chini ya Mkwasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’