Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema ushindi wa mabao 2-1 walioupata dhidi ya Lipuli Fc ni matokeo ya mpango walioingia nao kwenye mchezo huo
Akizungumza jana baada ya mchezo, Tshishimbi alisema walitawala kipindi cha kwanza na mpango wao ilikuwa kumaliza mchezo kwenye kipindi hicho
Hata hivyo walikosa nafasi nyingi pamoja na kutumia nafasi mbili zilizowapa mabao hayo mawili
"Lipuli ni timu nzuri, wana Physic nzuri sana. Mpango wetu ilikuwa ni kumaliza mchezo kipindi cha kwanza," alisema
"Tulipambana na kupata magoli mawili, kipindi cha Lipuli walipambana na kupata goli moja ambalo liliwaongezea kujiamini. Tunamshukuru Mungu tuliweza kumaliza mchezo huu kwa ushindi wa goli 2 - 1"
Ushindi huo umeipandisha Yanga mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 34
Mchezo unaofuata ni dhidi ya Ruvu Shooting na utapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa