Kuelekea mchezo dhidi ya Simba, Lwandamina hana presha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Oct 2017
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba, Lwandamina hana presha
Yanga inaingia katika mchezo wa keshokutwa dhidi ya Simba tofauti kabisa na ile iliyocheza August 23 kwenye Ngao ya Jamii.

Japo kikosi kinaweza kuwa kilekile lakini wakati ule bado Yanga ilikuwa haijaiva, naweza kusema ilikuwa bado haijakaa kitimu zaidi kama sasa.

Kwa sasa utaona falsafa ya kocha George Lwandamina tayari imepenya kwa kiasi kikubwa ndani ya akili za wachezaji.

Lwandamina sio mpenzi wa mpira wa kufurahisha jukwaa, mara nyingi hupendelea mpira ufike langoni kwa adui haraka iwezekanavyo ili uongeza nafasi ya kupachika mabao.

Wakati Falsafa ya Omog ikiwa tofauti. Simba inacheza kwa kupasiana zaidi kwa pasi fupifupi. Sasa inapokutana na timu zenye safu imara ya ulinzi kuanzia katikati mfumo huu hauwezi kufua dafu.

Angalia michezo ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar, Mbao FC na Azam FC. Hizi ni timu zinazojua kujilinda.

Hata katika mchezo wa Ngao ya Jamii licha ya kutawala mchezo kwa muda mwingi Simba haikuweza kufunga.

Mfumo huo pia hautafua dafu kwenye mchezo wa Jumamosi na hatari zaidi ni kwamba upo uwezekano wa Yanga kufunga mabao yake kupitia mashambulizi ya kushitukiza, mipira iliyokufa na hata kona.

Siku hiyo kazi kubwa ya viungo wa Yanga watakao-ongozwa na Tshishimbi itakuwa kuwapora mpira akina Niyonzima katikati na kuanzisha mashambulizi ya haraka kupitia akina Ajibu, Chirwa, Mwashiuya au Buswita.

Kikosi cha Yanga kimeimarika kiasi kwamba kocha George Lwandamina anaweza hata asiwatumie Kamusoko, Ngoma na Tambwe na bado ushindi ukapatikana.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Stand United, Pato Ngonyani alimudu vyema nafasi ya kiungo mkabaji huku Tshishimbi akionyesha umahiri wake kwa kuimudu vyema nafasi ya Kamusoko.

Hakika mchezo huo wa Jumamosi haumuumizi kichwa kabisa kocha George Lwandamina ambaye ana kila dalili ya kupata ushindi wake wa kwanza dhidi ya Simba.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
19m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’