Licha LA Galaxy kusitisha mkataba wake, mambo bado yanamuendelea vizuri beki wa zamani wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' baada ya kupata timu nyingine barani Ulaya
Ninja atasafiri kuelekea nchini Latvia kujiunga na timu ya FK Rigas inayoshiriki ligi kuu nchini humo
Beki huyo kutoka visiwani Zanzibar, Februari 15 atafanyiwa vipimo vya afya na atajiunga na timu hiyo kama kila kitu kitakwenda sawa
Awali Ninja alisajiliwa na MFK Vyskov ya Jamhuri ya Czech, hata hivyo hakuitumikia timu hiyo kwani alitolewa kwenda LA Galaxy kwa mkopo
ADVERTISE HERE