Kikosi cha Yanga jioni hii kinafanya maandalizi ya mwisho kwenye uwanja wa Chuo cha Utalii kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru
Furaha imetawala kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael ambaye kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kuirejesha timu kwenye makali yake
Mkongwe Kelvin Yondani sasa yuko fiti baada ya kukosekana dimbani kwa wiki kadhaa
Kesho anaweza kurejea dimbani kuikabili Ruvu Shooting
ADVERTISE HERE