Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) huenda itaiondolea Yanga adhabu waliyowapa baada ya mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Januari 04 kwenye uwanja wa Taifa baada ya kugoma kuingia kwaenye vyumba vya kubadilishia nguo
Kamati ya Saa 72 iliiadhibu Yanga kwa kuipigafaini ya Sh 200,000 baada ya kugoma kuingia kwenye vyumba hivyo kutokana na uwepo harufu kali isiyofahamika
Hata hivyo hivi karibuni timu za Mwadui Fc, Namungo na Polisi Tanzania nazo ziligoma kutumia vyumba hivyo kutokana na uwepo wa harufu hiyo
Juzi kwenye mchezo dhidi ya Lipuli Fc, kwa mara nyingine kocha mkuu wa Yanga, Lucy Eymael aliwazuia wachezaji kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai kuwa kulikuwa na harufu ambayo alihisi siyo salama kwa wachezaji wake.
Mwenyekiti wa Bodi la Ligi Tanzania Bara, Steven Mnguto amesema bodi yake itajiridhisha na uwepo wa madai hayo na kama yatathibitika, basi Yanga itafutiwa adhabu waliyopewa mwanzo
Aidha Mguto amesema watafanya uchunguzi wa kina ili kuwabaini waliohusika kuchafua vyumba hivyo na kuweza kuwachukulia hatua