Maamuzi mbalimbali ya Kamati ya saa 72

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2020
Maamuzi mbalimbali ya Kamati ya saa 72

Mwamuzi Abubakar Mturo amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kumudu mchezo katika mechi iliyochezwa Februari 05,2020 kati ya Yanga dhidi ya Lipuli Fc katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi

Polisi Tanzania imepigwa Faini ya Tsh.1,500,000/=(Milioni Moja na Laki Tano) kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi wa kuingia Uwanjani katika mechi iliyochezwa Februari 04,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar.

Adhabu hii imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(14) ya Ligi Kuu

Kocha wa Simba Sven Vanden Broeck amepewa Onyo Kali kwa kosa la kugoma kuwafungulia mlango mwamuzi na Kamishina wa mchezo wakati wa ukaguzi wa timu katika mechi hiyo iliyochezwa Februari 01,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 41(13) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.Maamuzi ya Kikao cha Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020

Katika hatua nyingine, kikao cha ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi kilichokaa Februari 10,2020 Kimeielekeza Sekretarieti kufuatilia viongozi wa vilabu na Makocha ambao hivi karibuni wamekuwa wakishutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi ,Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti tofauti

Viongozi na Makocha waliobainika ni wafuatao Kocha wa Klabu ya:- Namungo FC (Hitimana ), kwenye mchezo wa Simba SC na Namungo Fc,Β  Kocha wa Klabu ya Young African Sc (Luc Aymael), kwenye mchezo wa Yanga Sc na Lipuli, Msemaji wa Klabu ya Simba SC (Haji Manara) na Muhamasishaji wa Young African sc(Anthonio Nugaz) . Kutokana na matamshi hayo wanapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’