Nchimbi 'afagilia' kucheza na Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2020
Nchimbi 'afagilia' kucheza na Molinga

Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi, amemtaja David Molinga kuwa ndiye anayempa raha kila wanapocheza pamoja, ikiwa ni baada ya kutengeneza pacha hatari hivi karibuni

Tangu aliposajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwezi uliopita, Nchimbi ameonekana kuelewana vilivyo na straika Mkongo, Molinga, wakiisaidia timu yao hiyo kuendelea kukusanya pointi msimu huu.

Kombinesheni yao ilianza kuonekana katika mchezo wa Ligi Kuu kati ya Yanga na Mtibwa Sugar, Nchimbi akitoa asisti tamu kwa Molinga, pia, alikuja kufanya hivyo tena Wanajangwani walipomenyana na Ruvu Shooting.

Nchimbi maarufu kama Duma, amesema baada ya kucheza michezo michache sambamba na Molinga ameanza kuielewa mikimbio ya mshambuliaji mwenzake huyo na jinsi gani ya kumpenyezea pasi za kufunga mabao.

"Nafurahi mno ninapocheza na Molinga. Sasa nafahamu ni aina gani ya pasi za kumpenyezea na katika mazingira yapi ili aweze kufunga mabao.

"Uzuri ni kwamba Molinga ana uelewa mkubwa wa mchezo wa soka, hata kama hana kasi, lakini anajua aina ya pasi ninazomletea njiani kutokana na mimi pia nimeshafahamu nimchezeshe vipi"

Tangu ajiunge na Yanga, Nchimbi bado hajafanikiwa kuifungia bao, lakini uwezo wake wa kukaba na kukokota mpira unaonekana kuwa na faida ndani ya timu hiyo kupitia kwa wachezaji wenzake

Kesho Jumamosi Yanga itashuka dimba la Taifa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo wa ligi kuu mzunguuko wa 22

Yanga ilishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa mkoani Iringa

Baadae ikashinda 2-0 kwenye mchezo wa kombe la FA hatua ya 32 bora

Bila shaka Molinga na Nchimbi watajumuishwa kwenye kikosi kitakachoshuka dimbani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
11h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’