Mashabiki tukubali, tutoe nafasi ya kujenga timu

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
19 Feb 2020
Mashabiki tukubali, tutoe nafasi ya kujenga timu

Dalili zimeonekana kuwa Yanga huenda ikamaliza msimu wa tatu bila ya kupata ubingwa wa ligi kuu kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha

Lakini hili ni jambo ambalo baadhi ya wachambuzi walilitabiri kutokana na mabadiliko yaliyotokea Yanga msimu huu

Timu ilianza na kocha Mwinyi Zahera ambaye pia alifanya usajili wa wachezaji aliowahitaji

Lakini baada ya mechi takribani sita Zahera alitimuliwa akiwa amepoteza mchezo mmoja na sare moja kwenye ligi, matokeo ya kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho na Pyramids Fc yakitajwa kuwa sababu

Baada ya Zahera kuondoshwa Mkwasa akakabidhiwa timu ikielezwa angeongoza kwa wiki mbili wakati uongozi ukikamilisha mchakato wa kumpata kocha mpya

Hata hivyo Mkwasa akadumu kwa takribani miezi miwili kabla ya ujio wa kocha Luc Eymael

Wakati wa usajili wa dirisha dogo ni Mkwasa aliyetoa mapendekezo ya wachezaji aliotaka wasajiliwe na wakati huohuo Yanga ikiachana na tabribani wachezaji sita waliokuwa wamesajiliwa na Zahera

Kocha Eymael akakabidhiwa timu iliyoundwa na Mkwasa mwenyewe akipata nafasi ya kumsajili Bernard Morrison pekee

Ukiangalia mfululizo wa mabadiliko hayo kuanzia wachezaji na benchi la ufundi, ni dhahiri changamoto ya muunganiko wa timu ni lazima itokee

Eymael kwa kiasi kikubwa amejitahidi kuimarisha timu licha ya kuwa hana muda mrefu sana

Kwa hali ilivyo sasa ni vyema Eymael akaachwa aendelee kujenga timu bila ya kuwekewa presha na mashabiki

Kwani akiachwa afanye kazi, msimu ujao Yanga itakuwa imara sana. Ameona mapungufu yaliyopo hasa kwenye safu ya ushambuliaji, mwezi Juni atakuwa na kazi rahisi kusajili wachezaji wa kuziba mapengo hayo

Lakini uamuzi wowote wa mabadiliko mengine ya benchi la ufundi kipindi hiki, utaivuruga zaidi Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’