Kilio cha Wanayanga kiko hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2020
Kilio cha Wanayanga kiko hapa

Hakuna shabiki wa Yanga anayeweza kufurahia mwenendo wa timu wakati huu, sare tatu mfululizo sio matokeo ya kufurahiwa

Wengi wametoa maoni yao kwa kile ambacho wanadhani kikifanyiwa kazi na benchi la ufundi, manufaa yanaweza kupatikana

Benchi la ufundi lina nafasi ya kuchambua na kufanyia kazi yale ambayo wengi wanadhani inafaa yarekebishwe

Maoni mengi yametolewa, baadhi yake ni haya;

1. SAFU YA ULINZI

Kumekuwa na mtazamo tofauti kuhusu safu ya ulinzi wa Yanga, hasa pacha ya walinzi wa kati

Wakati Lamine Moro akicheza sambamba na Said Juma Makapu huku mlinda lango akiwa Metacha Mnata, Yanga iliweza kucheza takribani mechi tatu bila ya kuruhusu bao

Lakini pacha ya Shikhalo, Lamine na Yondani imekuwa ikiruhusu mabao mara kwa mara

Wapo wanaohoji Andrew Vicent na Ally Ally kwa nini hawapewi nafasi?

Ukizungumzia mabeki mahiri wa kucheza mipira ya juu kwenye kikosi cha Yanga ni Lamine Moro, Andrew Vicent na Ally Ally

Yanga ilisitisha mpango wa kumtoa kwa mkopo Ally Ally lakini haonekani kuwa na nafasi kwenye kikosi cha kwanza

2. Mfumo wa 4-4-2 unaweza kuwa bora

Kocha Luc Eymael anapendelea zaidi mfumo wa 4-2-3-1 ambapo anatumia mshambuliaji mmoja mbele

Hata hivyo Yanga haionekani kufunga mabao mengi kupitia mfumo huo

Msimu huu imefunga mabao 25 na kuruhusu mabao 18, wastani wa chini sana kuonekana kwenye miaka ya karibuni

Pengine kuanza na washambuliaji wawili inaweza kuwa na manufaa

David Molinga, Tariq Seif na Ditram Nchimbi wanaweza kupokezana nafasi mbili za ushambuliaji huku Patrick Sibomana, Deus Kaseke na Mrisho Ngasa wakarejeshwa majukumu ya ushambuliaji wa kutokea pembeni

Eymael anamtumia Nchimbi winga ya kulia hivyo kumuondoa kikosi cha kwanza Patrick Sibomana ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji tegemeo wakati wa Zahera na Mkwasa

3. Patrick Kabamba haonekani

Wakati wa dirisha dogo Yanga ilimsajili winga Patrick Kabamba kutoka klabu ya Buildcon Fc ya nchini Zambia

Kabamba alisajiliwa baada ya kufuzu majaribio

Hata hivyo mchezaji huyo bado hajaonekana kikosini wengi wakiwa na shauku ya kumuona akipewa nafasi

4. Yikpe bado

Ukweli ni kwamba mshambuliaji Yikpe Gnamien ameshindwa kuwashawishi Wanayanga licha ya kuwa amefunga mabao mawili tangu asajiliwe dirisha dogo

Eymael ana imani kuwa mshambuliaji huyo atakuwa sawa, lakini uvumilivu umeanza kuwashinda mashabiki

Mbelgiji huyo amekiri Yikpe raia wa Ivory Coast kuwa na mapungufu huku akiahidi kumsaidia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’