Mchezaji wa Yanga SC Bernard Morrison amepelekwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Tanzania Prisons FC Jeremia Juma wakati mpira ukiwa umesimama kwenye mchezo uliofanyika Februari 15, 2020 uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
Wakati TFF ikichukua hatua hiyo kwa Morrison, wadau wa soka bado wanajiuliza kwa nini tukio la mlinzi wa Simba Paschal Wawa kumkanyaga makusudi Ditram Nchimbi Januari 04 hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa mpaka leo
Aidha tukio la kupiga kiwiko pia lilifanywa na mshambuliaji Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Prisons
Kama lilivyo tukio la Morrison, matukio yote yalinaswa na kamera za Azam TV
Uamuzi huu huenda ukaibua mjadala mkali hasa ikitokea Morrison atazuiwa kucheza mchezo dhidi ya Simba March 08
Kama atapatikana na hatia, Morrison atafungiwa mechi tatu
Lakini muhimu TFF ilipaswa kuchukua hatua kwa matukio yote ya aina hiyo bila ya kujali yamefanywa na nani na sio kubagua