Ukizungumzia Yanga ile ya wakati wa Manji ambayo ilikuwa ikitesa sana, hutakosa kutaja jina la Jery Muro wakati huo akiwa Afisa habari na Msemaji wa timu
Muro amerejea Yanga kuweka mambo ya hamasa sawa hasa wakati huu ambao timu imekabiliwa na changamoto ya kupata matokeo
Ameanza rasmi kazi leo kwa kushirikiana na kina Hassan Bumbuli na Antonio Nugaz kuelekea mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao utapigwa March 08 kwenye uwanja wa Taifa
Ameanza kwa kuwapa ujumbe mashabiki wa Simba wakiongozwa na Msemaji wao Haji Manara ambao wamekuwa wakishangilia matokeo ya sare ambayo Yanga imepata mechi za hivi karibuni
"Hao wanaohoji mbona sare zimekuwa nyingi muwape taarifa, muwaambie kuwa tarehe nane tunaoa...!"
ADVERTISE HERE