Baada ya Jery Muro kutoka Yanga takribani miaka mitatu iliyopita, msemaji wa Simba Haji Manara ni kama alikosa mpinzani na alitamba vile alivyotaka
Muda mwingi ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuitania na wakati mwingine kutupia madongo na kashfa za hapa na pale kwa chochote kinachofanywa na Yanga
Leo 'mbabe' wake Jery Muro ametangaza kurejea Yanga japo ni kwa muda mfupi
Enzi za Muro, Manara alikosa la kusema ilifikia wakati alitishia kwenda kumshitaki Muro Mahakamani baada ya kushindwa kuhimili madongo aliyokuwa akitupiwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru
Hata hivyo wawili hao nje ya uwanja ni marafiki ambapo hata wakati Manara alipokuwa akisumbuliwa na matatizo ya macho, Muro alipitisha Harambee kwa mashabiki wa Yanga ambao walimchangia na akaweza kwenda kutibiwa India
Muro amerejea na kumtaka Manara ajitafakari kwani amen'gan'gania katika nafasi hiyo ya usemaji bila ya kuwaachia wengine
Muro amesema yeye alipomaliza muda wake Yanga aliondoka na kuwapisha wengine sasa kijiti kikiwa mikononi mwa Antonio Nugaz na Hassan Bumbuli
"Uongozi ni kupokezana vijiti, nimeondoka nimewaachia akina Nugaz, kuna ndugu yangu yupo tu ameng'ang'ania kama kigando au ni msukule wa Simba ? au hana kazi nyingine ya kufanya? rudi kafundishe madrasa maana ndio elimu pekee uliyonayo. na akiongea ongea ovyo asisahau kuwa mi mkuu wa wilaya ntamuweka ndani masaa 48," alisema Muro
Aidha Muro amesema amerejea Yanga kwa lengo la kuongeza hamasa na kuwaunganisha wadau wote wa klabu hiyo ili kuhakikisha wanarejesha ufalme wao kwa soka la Tanzania
"Nipo hapa kuwatangazia wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa jumla kuwa huu ndio muda rasmi wa Yanga, ile kampa kampa tena inarudi. . Password tunazo sisi na tayari nishampa katibu na kocha wetu . ."
"Tutapambana na yeyote anayetaka kuionea ama kuidhurumu Yanga. Viongozi mliokuwepo rudini tuungane , mimi nimekuja hakuna aliyeniita nimeona fedheha ,karaha zimezidi. . Ukuu wa wilaya ulinikuta nikiwa Yanga SC . . Usisubiri kuitwa wala kuchaguliwa katika kamati kama unaumia na Yanga njoo. .
"Mkemi, Kleb na wengineo tunajuana wale wazee wa kamati ya miba. .Njooeni tusikae pembeni kulalamika, njoeni tuungane milango ipo wazi viongozi nishaongea nao hawana hiyana na hawawezi mzuia mtu"