FT : Yanga 1-1 Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2017
FT : Yanga 1-1 Simba
Mpambano wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba uliopigwa leo kwenye dimba la Uhuru umemalizika kwa sare ya bao 1-1.

Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu ulizishuhudia timu zote zikicheza vizuri kwa nyakati tofauti huku Simba ikiwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lililofungwa na Shiza Kichuya.

Kichuya alitumia makosa ya walinzi wa kati wa Yanga pamoja na kipa Youthe Rostand waliotegeana kuondosha krosi ya Emanuel Okwi.

Hata hivyo bao hilo halikudumu kwani Kwenye dakika ya 60 Orey Chirwa aliyekuwa anaichachafya sana ngome ya Simba aliunganisha vizuri krosi ya Geofrey Mwashiuya aliyewatoka Erasto Nyoni.



Kuingia kwa bao hili kuliiamsha Yanga iliyopeleka mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba.

Emanuel Martin aliyeingia kuchukua nafasi ya Mwashiuya alikosa bao la wazi baada ya kubaki yeye na mlinda lango Aishi Manula kwenye dakika ya 69 ambapo shuti lake liliokolewa na Manula aliyekuwa kikwazo kikubwa kwa mashambulizi ya Yanga.

Licha ya tambo nyingi za Simba kwa mara nyingine kikosi cha Yanga kilichokuwa bila wachezaji wake waliokuwa wakitajwa sana, Tambwe, Ngoma na Kamusoko, Yanga iwezesha kudhirisha kuwa ubingwa msimu wa nne unawezekana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’