FT : Yanga 2-0 Alliance Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Feb 2020
FT : Yanga 2-0 Alliance Fc

Mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kushuhudia mtanange wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Alliance, wamepata burudani ya kutosha kutoka kwa mabingwa wa kihistoria Yanga ambao walitakata kwelikweli katika mchezo huo ambao Yanga imepata ushindi wa mabao 2-0

Mabao yote ya Yanga yaliwekwa kambani na Ditram Nchimbi ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Tariq Seif

Nchimbi sasa amefikisha mabao sita, akifungua ukurasa wa kuzifumania nyavu ndani ya uzi wa Yanga

Vijana wa Luc Eymael walikuwa bora sana katika mchezo huo ambao waliwavuruga kwelikweli Alliance waliokuwa wakiusaka mpira kwa tochi muda mwingi wa mchezo

Kwa mara nyingine waamuzi walimnyima Bernard Morrison mikwaju miwili ya penati baada ya kufanyiwa madhambi dhahiri ndani ya eneo la hatari

Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya kupata sare nne mfululizo

Yanga pia haijaruhusu bao lolote katika michezo hiyo miwili

Jumanne Yanga itarejea uwanja wa Taifa kuumana na Mbao Fc

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
56m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’