Kikosi cha Yanga kesho Jumanne, March 03 kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Mbao Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Alliance Fc juzi, hii ni nafasi nyingine kwa Yanga kuendelea kujizatiti kwenye msimamo wa ligi
Lakini pia, mchezo huu ni sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa March 08
Yanga tayari imeweka hadharani viingilio vya mchezo huo ambapo VVIP ni Tsh 15,000/-, VIP B na C ni Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Ni nafasi nyingine kwa mashabiki kwenda kushuhudia burudani kutoka kwa mabingwa hao wa kihistoria
Mchezo utapigwa saa moja jioni
ADVERTISE HERE