Yanga yaita mashabiki mechi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Mar 2020
Yanga yaita mashabiki mechi dhidi ya Simba

Uongozi wa klabu ya Yanga umetaka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, March 08 kwenye uwanja wa Taifa

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Afisa habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema timu inaendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo huo

Amesema wote wako katika hali nzuri ispokuwa winga Juma Mahadhi ambaye ameanza mazoezi hivi karibuni baada ya kupona majeraha ya goti yaliyomuweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja

"Wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo isipokuwa Juma Mahadhi ambaye bado hayuko sawa kiafya"

"Tunawataka mashabiki waje kwa wingi watuunge mkono katika mchezo huu ambao sisi ni wenyeji. Wakifika uwanjani waanze kukaa majukwa ambayo wapinzani wetu hukaa kwani huu ni mchezo wetu, tunaweza kujipangia utaratibu wa kukaa tunaotaka," amesema

Aidha Bumbuli amesema kuelekea mchezo huo Yanga hawatahamisha kambi yao iliyopo Regency Hotel, pia wataendelea kufanya mazoezi yao viwanja vya Chuo cha Sheria, jambo kubwa walilofanya ni kuongeza ulinzi

GSM kutoa Milioni 200

Katika hatua nyingine, GSM wameahidi kutoa kitita cha Tsh Milioni 200 za hamasa ili Yanga iweze kushinda

Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amethibitisha kuwa ahadi hiyo tayari imewasilishwa na wadhamini wao hao wanaohusika na kutengeneza na kusambaza jezi za klabu ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’