Tunawaheshimu Simba lakini Jumapili hawatoki - Nugaz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2020
Tunawaheshimu Simba lakini Jumapili hawatoki - Nugaz

Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amesema kikosi cha timu hiyo kiko tayari kwa mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa

Msemaji huyo wa Yanga amesema kocha Luc Eymael tayari ameandaa mbinu za kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo

Nugaz amesisitiza kuwa Yanga haitaingia kama 'undar-dog', wanatambua kuwa Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri lakini siku hiyo watakumbana na Yanga ambayo hawajawahi kuiona

"Sisi hatutaingia kama under-dog kama wanavyosema wengine, tunaiheshimu timu yao pamoja na wachezaji wao lakini siku hiyo tutawachezea mpira ambao hawajawahi kuuona," ametamba Nugaz

"Tunafahamu udhaifu wao uko wapi ndio maana hata kocha wetu amesema hana wasiwasi kabisa kuwakabili Jumapili"

"Mashabiki wetu waje uwanjani kwa wingi, wajiamini na watembee kifua mbele kwani siku hiyo Mnyama hana pa kutokea"

Huu utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Luc Eymael na anaweza kuweka rekodi mpya kama ataiongoza Yanga kupata ushindi

Baada ya password ya ushindi kuletwa na Jerry Muro, pengine siku ya Jumapili itakuwa siku ya furaha kwa mashabiki wa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’