Moja ya mambo yaliyowagusa wengi ni picha ya huyo kijana alionyesha mapenzi ya dhati kwa kiungo mcongo wa Yanga Papi Kabamba Tshishimbi.
Dogo huyu ambaye taarifa zake zinasakwa ameandika jina la kiungo huyo katika shati yake kuukuu.
Mwenye taarifa sahihi kuhusu kijana huyu aziweke hadharani ili aweze kupatiwa jezi mpya ya Yanga yenye jina la Papi Tshishimbi.
Utaratibu huu wa 'kutoa shukrani' kwa vijana hawa wenye mapenzi na wasakata kabumbu licha ya kuwa na hali duni umeasisiwa na Lionel Messi ambaye alimwalika Barcelona kijana kutoka Afghanistani baada ya kuona picha zake kwenye mitandao ya kijamii akiwa amevaa mifuko ya rambo yenye mistari sawa na jezi za timu ya Taifa ya Argentina huku nyuma yake akiwa ameandika namba 10 pamoja na jina la Messi.
Hivi karibuni kijana mwingine alizawadiwa jezi ya Donald Ngoma hukumsimu uliopita klabu ya Simba ikimzawadia jezi kijana aliyeandika jina la Ibrahim Ajib katika shati yake huko mkoani Dodoma.

ADVERTISE HERE