Mwakalebela atamba, bado Yanga inawania ubingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2020
Mwakalebela atamba, bado Yanga inawania ubingwa

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema bado timu yake iko kwenye mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 50, imezidiwa na Simba alama 18

Hata hivyo Yanga ina michezo miwili kibindoni ambayo kama watashinda yote watapunguza tofauti ya pointi hizo na kuwa 12

Mwakalebelela amesema Yanga bado ina michezo 13 wakati Simba wana michezo 11 hivyo hawawezi kusema mbio za ubingwa zimemalizika

"Bado mechi zipo nyingi, tunachopaswa kufanya ni kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye michezo yetu yote iliyobaki. Kwanye mpira wa miguu jambo lolote linaweza kutokea hivyo hatupaswi kukata tamaa," amesema Mwakalebela

Keshokutwa Alhamisi Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kumenyana na KMC kisha kuelekea Ruangwa mkoani Lindi kuwakabili Namungo Fc ukiwa ni mchezo wa kwanza baina ya timu hizo msimu huu ambao utapigwa March 15

Yanga pia bado haijacheza na Mwadui FC msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’