Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison hatarajiwi kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Namungo Fc kesho kutokana na majeraha
Morrison alikosa mchezo ddhidi ya KMC kutokana na majeraha hayo ambayo aliyapata kabla ya mchezo dhidi ya Simba uliopigwa March 08
Morrison amepewa mapumziko maalum ili aweze kupona kabisa kabla ya kurejea tena dimbani
Mghana huyo huenda akaanza kuonekana kikosini mwezi ujao baada ya mapumziko ya mechi za Kimataifa
Hata hivyo kuna uwezekano akarejea mapema zaidi iwapo TFF itaamua kuendelea na ratiba ya ligi baada ya CAF kusitisha mechi za Kimataifa zilizokuwa zipigwe mwishoni mwa mwezi huu kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona
Kuna uwezekano mkubwa michuano ya CHAN ambayo ilipangwa kuanza April 05 mpaka April 25 nayo haitafanyika