Mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Corona ambao umeingia nchini
Morrison amesema ni muhimu kwa kila mmoja kuzingatia na kufuata taratibu za kiusalama zinazoelekezwa ili kuepuka maambukizi
"Kwa mashabiki wetu wa Yanga tunawahitaji kutuunga mkono ili tuendelee kupambana hivyo tunawahitaji muwe hai"
"Fuateni taratibu za kiusalama, safisheni mikono yenu na tumieni vifaa kama 'Sanitizer' "
"Jilindeni pamoja na familia zenu kuhakikisha hawapati maambukizi ya ugonjwa huu," amesema Morrison
Juzi Morrison alilazimika kujitenga na wachezaji wengine baada ya kuonyesha dalili za ugonjwa huo
Hata hivyo mwamba huyo kutoka Ghana yuko salama
ADVERTISE HERE