Huyu Balama akikomaa atafika mbali - Niyonzima

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Apr 2020
Huyu Balama akikomaa atafika mbali - Niyonzima

Kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima ameeleza kuvutiwa na uchezaji wa kiungo anayecheza nae kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria, Mapinduzi Balama

Niyonzima aliyerejea Yanga mwezi Januari, amesema Balama ni mmoja wa wachezaji bora aliowahi kucheza nao

"Navutiwa sana na uchezaji wa Mapinduzi Balama. Nafikiri akiendelea kujituma atapata mafanikio makubwa sana. Ni mchezji mwenye kipaji na anapokuwa uwanjani anafahamu vyema majukumu yake," amesema Niyonzima

Niyonzima aliongeza kuwa bao alilofunga nyota huyo kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Simba Januari 04 mwaka huu, ni miongoni mwa mabao bora yaliyofungwa msimu huu

Balama aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Alliance Fc, ameanza vyema maisha yake Jangwani akijihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza licha ya mabadiliko ya makocha watatu

Kiwango chake kimempa nafasi ya kuitwa kikosi cha timu ya Taifa kilichopaswa kushiriki michuano ya CHAN nchini Cameroon ambayo hata hivyo iliahirishwa kutokana na janga la Corona

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’