Yanga washindwe wenyewe kwa Kaheza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Apr 2020
Yanga washindwe wenyewe kwa Kaheza

Yanga washindwe wenyewe kwa Marcel Kaheza baada ya klabu ya Polisi Tanzania, kusema kuwa hawatakuwa na tatizo naye iwapo Wanajangwani hao watakubaliana na winga huyo ili kutua Jangwani.

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, aliwahi kusema kwamba wanapocheza na Polisi Tanzania, huwa anamuhofia mno Kaheza kutokana na umahiri wake uwanjani.

Baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimamishwa kutokana na hofu ya kuenea kwa maambukizi ya virus vya Corona, Yanga walidaiwa kuwa katika mkakati wa kumuwania wingi huyo wa zamani wa Simba ili kukiimarisha zaidi kikosi chao.

Kocha wa Polisi Tanzania, Hamsini Malale, amesema kuwa hatakuwa na shida iwapo Yanga itamtaka Kaheza kwani ana uwezo wa kutengeneza wachezaji wengine na kuwafanya kuwa bora zaidi na hivyo kukisaidia kikosi chake.

"Wanaohusishwa na timu kubwa katika kikiosi changu ni wengi, unajua hizi timu kubwa zikitaka wachezaji, haziwezi kuwakosa, iwapo wataondoka, sitakuwa na shida nao, siwezi kuwazuia, nitawaruhusu tu na kutengeneza wengine," amesema.

Mbali ya Kaheza, mchezaji mwingine wa Polisi Tanzania anayetolewa macho ni na klabu za kadhaa za Ligi Kuu Bara ni Sixtus Sabilo aliyefanya vizuri msimu huu, akitajwa kuwaniwa na Simba.

Tayari Yanga ilishang’oa mchezaji Polisi Tanzania kipindi cha dirisha dogo ambaye ni mshambuliaji Ditram Nchimbi ambaye ameshajitengenezea jina Jangwani

Yanga pia inahusishwa kumuwania beki wa kushoto wa timu hiyo Yasin Mustafa

Bingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’