Corona yamkwamisha Eymael Ubelgiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2020
Corona yamkwamisha Eymael Ubelgiji

Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael aliyetarajiwa kurejea nchini juzi, amekwama Ubelgiji kutokana na kasi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Kutokana na ukubwa wa janga la ugonjwa huo, safari nyingi za ndege zinazotoka moja kwa moja Ulaya kwenda Afrika zimesitishwa na sasa anafikiria kusafiri hadi Ujerumani katika jiji la Frankfurt kuungaunga ndege hadi Misri kisha Ethiopia.

Eymael aliyekwenda kwao kuoa baada ya Ligi Kuu Tanzania Bara kusimamishwa kwa sababu ya janga la virusi vya corona, akirejea nchini pia anatarajiwa kukaa karantini kwa siku 14

Amesema baada ya kushindwa kuondoka juzi kama alivyopanga, sasa anafanya utaratibu wa kupata tiketi, ingawa anakiri kuwa ni ngumu kurudi nchini kwa ajili ya kuendelea kuifundisha Yanga.

"Hakuna ndege zinazoingia Ubelgiji kutoka Afrika kwa sasa zote zimezuiliwa kutokana na virusi vya corona na suluhisho langu kwa sasa nitasafiri hadi Ujerumani kwenye mji wa Frankfurt nitachukua ndege zinazoenda Misri kisha nitasafiri hadi Ethiopia na kuunganisha tena ndege hadi Dar es Salaam na safari yangu itadumu kwa wiki moja, " Eymael amenukuliwa na Habari Leo

Amesema baada ya kufuata utaratibu wa hapa nchini ambao umepangwa na serikali, kitu cha kwanza atakapoingia Yanga atakutana na viongozi wa timu hiyo na kuangalia wachezaji walioongezewa mikataba na kisha kuangalia mapendekezo ya mahitaji ya nyota wapya anaotaka kuwasajili kuimarisha kikosi hicho msimu ujao kama yamefanyiwa kazi.

Eymael alisema mafaili yote ya mahitaji ya msingi ambayo anahitaji kuboresha kikosi hicho alishawaachia viongozi ili kutimiza makubaliano waliyofanya ili kuhakikisha timu hiyo inakuwa bora zaidi na kutwaa ubingwa msimu ujao.

“Nawaamini viongozi pamoja na mdhamini GSM, yote yataenda sawa na nikifika lazima tufanye kikao cha mrejesho wakati tunasubiri taarifa kutoka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhusu ratiba ya kumalizia michezo iliyosalia ya Ligi,” alisema.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’