Yikpe kupewa nafasi kudhihirisha ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Apr 2020
Yikpe kupewa nafasi kudhihirisha ubora wake

Benchi la ufundi la Yanga linaloongozwa na kocha Mbelgiji Luc Eymael limepanga kutumia mechi zilizobaki za ligi kuu ya Vodacom kuwapa nafasi baadhi ya wachezaji ambao wamewekwa kwenye mpango wa kutemwa na timu hiyo, imefahamika

Miongoni mwa wachezaji hao ni mshambuliaji Yikpe Gnamien ambaye alitua dirisha dogo akiwa mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na Gor Mahia

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimebainisha kuwa Eymael amepanga kumtumia Yikpe kwenye mechi hizo kabla ya kuchukua maamuzi juu yake

Yikpe ameifungia Yanga mabao mawili tu tangu ajiunge nayo mwezi Januari

Sehemu kubwa ya mashabiki wa Yanga wamepoteza imani kwake wakitaka mkataba wake uvunje

Hata hivyo Eymael bado anaonekana kuwa na imani na mshambuliaji huyo ambapo kwenye moja ya mahojiano yake, alidai matatizo ya Yikpe yanarekebishika

Mu Ivory Coast huyo yuko nchini akiendelea kufanya mazoezi binafsi wakati huu ambao ligi imesimama kutokana na janga la corona

Uongozi wa Yanga umepanga kusajili safu mpya ya ushambuliaji ambapo inaelezwa ni mshambuliaji mmoja tu wa kati (Ditram Nchimbi) ambaye ana uhakika wa kuendelea kubaki msimu ujao

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
16h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’