Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi ameeleza kuvutiwa na kiungo wa Azam Fc Salum Abubakar 'Sure Boy' ambapo amesema kama Yanga itaweza kumnasa nyota huyo, msimu ujao watatisha
Sure Boy ni miongoni mwa nyota wazawa waliopendekezwa kwenye usajili wa kocha Luc Eymael

Hata hivyo kiungo huyo wa timu ya Taifa bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Azam Fc
Yanga italazimika kumalizana na Azam kabla ya kuipata saini yake
"Huyu kijana anajua sana, mimi namkubali. Akiwa uwanjani anatulia, anafanya majukumu yake ipasavyo, " Tshishimbi amenukuliwa na Mwanaspoti
GSM wametengeza zaidi ya Bilioni 1.5 kwa ajili ya kuisuka upya Yanga ambao mabilionea hao wameahidi kuwasajili wachezaji wote waliopendekezwa na Eymael
ADVERTISE HERE