Yanga, GSM mambo yamezidi 'kunoga'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Apr 2020
Yanga, GSM mambo yamezidi 'kunoga'

Klabu ya Yanga imesaini mkataba wa miaka miwili (2) na wadhamini wao kampuni ya GSM, mkataba unaoifanya GSM kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya klabu hiyo.

Awali GSM ilisaini mkataba na Yanga kwa ajili ya kuzalisha na kuuza jezi tu, mkataba ambao bado upo hadi sasa. Mkataba huu mpya utawafanya mashabiki na wanachama wa Yanga kupata bidhaa nyingine kama track suits, bukta/pensi, scarfs, t-shirts, vikombe, key holders na vingine vingi.

Eng. Hersi Saidi amesema wanafurahi kupata fursa ya kutengeneza bidhaa nyingine zaidi kwa ajili ya klabu ya Yanga. Amesema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa bidhaa nyingine tofauti ukiachana na jezi.

"Tukiwa kama wadhamini tunapenda kuona Yanga ikipata mapato zaidi kupitia nembo yao. Kwa muda mrefu sasa klabu imekuwa ikipoteza mapato ambayo yamekuwa yakiishia kwenye mikono ya watu wachache"

"Kwanza fikiria ni jezi ngapi zimeuzwa bila klabu kufaidika na matumizi ya nembo yao? Kumbuka wakati huo klabu ilikuwa inapata wakati mgumu kupata fedha kutoka vyanzo tofauti ili kuendesha shughuli zake za kila siku"

Ameongeza kuwa, GSM wanataka kuiona Yanga ikiwa imara kiuchumi.

"Tunahitaji kunufaika pia na udhamini wetu. Unawezaje kuuza bidhaa za klabu wakati mashabiki na wanachama hawafurahishwi na matokeo? Kwa hiyo matokeo mazuri ya timu yataleta chachu kwenye mauzo ya bidhaa za klabu hivyo watafurahia uwekezaji wetu"

Hata hivyo Hersi amesema mashabiki na wanachama wameanza kuwa na imani na timu yao na kuona sasa inaweza kupigania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara au Kombe la Azam Federation Cup (FA) kwa msimu huu.

hata hivyo Eng. Hersi ameeleza kuwepo kwa changamoto ya wazalishaji wa jezi feki

Amesema bado kuna mashabiki wananunua jezi ambazo hazina ubora kutoka kwa mawakala wasio na vibali jambo ambalo limekuwa tatizo licha ya wao kuchukua hatua za kisheria kwa wauzaji wa jezi feki.

Kwa mujibu wa Hersi, bado wanatafuta njia ya kuzuia watu wanaozalisha jezi feki na kuziuza lakini pia akatoa wito kwa mashaki kuacha kununua jezi feki ambazo hazina ubora kwa sababu kuendelea kufanya hivyo ni kuikosesha klabu mapato.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’