Yanga yakomalia mazoezi ya nyota wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Apr 2020
Yanga yakomalia mazoezi ya nyota wake

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredric Mwakalebela amesema kuwa wanaendelea kuwasimamia wachezaji wao kuhakikisha wanafanya mazoezi majumbani kwao ili kuwa tayari wakati wowote pale watakapohitajika

Ligi imesimama kwa zaidi ya mwezi mmoja kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona ambapo Serikali imeendelea kuchukua hatua kudhibiti ugonjwa huo

Serikali ilisitisha shughuli zote za michezo March 17 ambapo wiki iliyopita Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa alisema katazo hilo litaendelea hadi pale itakavyotangazwa vinginevyo

Mwakalebela amesema Yanga inasubiri mwongozo kutoka kwa Mamlaka husika lakini wanawasisitizia wachezaji wao kuwa wanapaswa kuwa tayari kwani jambo lolote linaweza kutokea

"Tunasubiri mwongozo, lakini ni lazima tuwe tayari kwa lolote, la kwanza ni kwamba msimu haujamalizika, hivyo wachezaji lazima wawe tayari kumalizia mechi zilizobakia, benchi la ufundi linasimamia vema na ninaamini hakuna aliyebweteka," aliongeza

Jana Shirika la Afya duniani (WHO), lilitoa mapendekezo kwa ligi zote kusitishwa hadi mwaka 2021 ambao ni matarajio kuwa janga la corona litakuwa limemalizika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’