Kuelekea msimu mpya, uongozi wa Yanga ya jijini Dar es Salaam, umesema wameongeza umakini katika mchakato wa usajili na sasa wataufanya kimya kimya kwa sababu wanataka kukamilisha mipango yao yote waliyoiweka
Hivi karibuni Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela aliingia matatani na uongozi wa Simba baada ya kudai kuwa Yanga ilikuwa kwenye mazungumzo na kiungo wa timu hiyo Clatous Chama
Simba ilipeleka malalamiko TFF ikidai kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba wa zaidi ya mwaka mmoja ingawa baadae Mwakalebela alifichua alikuwa akitania
Mwakalebela amesema kwa sasa hawataweka wazi michakato yao mpaka pale dirisha la usajili litakapokuwa limefunguliwa na kuwa wamekamilisha taratibu zote
"Tunajipanga kimya kimya, tutasajili kimya kimya, tunajua lolote linaweza kutokea ndani au nje yetu, hatutaki kuharibu mipango yetu," alisema Mwakalebela
Yanga inatarajiwa kuwa 'busy' kwenye dirisha la usajili baada ya wadhamini wao GSM kuahidi kukisuka upya kikosi cha timu hiyo