Mhilu, Matheo waliondoka mapema Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2020
Mhilu, Matheo waliondoka mapema Yanga

Mshambuliaji wa Kagera Sugar Yusufu Mhilu anashika nafasi ya pili katika mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa amefunga mabao 11 sawa na Reliants Kusajo wa Namungo Fc

Nyota hao wanamfukuzia mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere aliyepachika mabao 19 msimu huu

Mhilu ni zao la klabu ya Yanga kwani alilelewa kwenye kikosi cha timu ya vijana kabla ya kupandishwa kikosi cha kwanza na Hans van Pluijm mwaka 2016

Mhilu alikuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Yanga wakati wa kocha George Lwandamina lakini alipokuja Mwinyi Zahera pasipo kutarajiwa, alipendekeza mchezaji huyo atolewe kwa mkopo klabu ya Ndanda FC wakati huo akiwa amebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Yanga

Baada ya mkopo huo kumalizika Zahera hakuonekana kuvutiwa nae tena na hivyo akaamua kujiunga na Kagera Sugar

Lakini kwa mambo anayofanya Kagera Sugar, ni dhahiri uongozi wa Yanga unaweza kujilaumu kwa kukubali nyota huyo akaondoka kirahisi

Msimu huu Mhilu amekuwa kwenye kiwango bora sana katika klabu ya Kagera Sugar

Matheo Anthony ni nyota mwingine ambaye pengine alipaswa kupewa muda zaidi Yanga

Anthony alijiunga na Polisi Tanzania usajili wa dirisha dogo na kwa muda mfupi ameonekana kuwa mmoja wa washambuliaji tishio ligi kuu ya Vodacom

Hawa ni wachezaji ambao wamekulia kunako klabu ya Yanga lakini pengine uongozi ulifanya papara kuwaruhusu waondoke huku badala yao, wakisajiliwa wachezaji ambao uwezo wao ni wa kawaida

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’