Mmachinga : Ifahamu rekodi yake ya mabao 26 iliyodumu miaka 26

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Apr 2020
Mmachinga : Ifahamu rekodi yake ya mabao 26 iliyodumu miaka 26

Mohammed Hussein 'Mmachinga' nyota wa zamani wa Yanga, anashikilia rekodi ya kupachika mabao ligi kuu ya Tanzania Bara

Ilikuwa mwaka 1994 ambao Mmachinga aliweka rekodi hiyo kwa kupachika mabao 26 katika msimu mmoja

Sasa ni miaka 26 imepita tangu aandikishe rekodi hiyo..!

Lakini jambo moja kubwa ambalo linaifanya rekodi yake kuwa ya kipekee, ni kuwa mabao yake yote aliyafunga kawaida

Katika msimu huo Mmachinga hakuwahi kupiga mkwaju wa penati

Lakini pia, ikumbukwe wakati huo ligi ilikuwa ikishirikisha timu 16 tu

Mwaka 2006, Abdallah Juma wa Mtibwa Sugar alikaribia kuifikia rekodi hiyo baada ya kuifungia timu yake mabao 25

Hata nyota wa kigeni wameshindwa kuivunja rekodi hiyo ambapo Amissi Tambwe alifunga mabao 21 wakati akiwa Yanga na Meddie Kagere msimu uliopita aliifungia Simba mabao 23

Msimu huu Kagere amefunga mabao 19, anahitaji kufunga mabao sita katika mechi zilizobaki

Hata hivyo katika mabao yake, mengine ameyafunga kupitia mikwaju ya penati tofauti na Mmachinga ambaye hakuwa akipiga penati

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
20m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’