Uongozi wa klabu ya Yanga umelazimika kuahirisha Mkutano Mkuu wa Wanachama uliopaswa kufanyika mwezi huu kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona ambao ni tishio kote duniani
Jana katika uzinduzi wa Jarida la Yanga, Mwenyekiti wa mabingwa hao wa kihistoria Dk Mshindo Msolla alisema mazingira ya sasa hayaruhusu kufanyika kwa Mkutano huo hivyo wameu-ahirisha mpaka hapo Kamati ya Utendaji itakapotangaza tarehe nyingine pale mambo yatakapotulia
Aidha kuhusu mwenendo wa mchakato wa mabadiliko, Dk Msolla alisema Kamati iliyoundwa na klabu kusimamia mchakato huo inaendelea na majukumu yake ambapo tayari wametoa andiko la kwanza kuhusu mfumo wa uendeshaji uliopendekezwa
Andiko hilo linapitiwa na wadau mbalimbali
Dk Msolla alisema mchakato huo utawashirikisha wadau wote wa klabu ya Yanga ambapo viongozi wa Matawi watapewa semina ya muundo mpya wa uwekezaji kisha kuwaelimisha Wanachama na mashabiki kupitia Matawi yao
Kuhusu ushirikiano na La Liga, Dk Msolla amesema tayari wamepokea rasmi ya kwanza ya mkataba ambapo kwa sasa wadau wanaupitia kabla ya hatua ya kusainiwa kufanyika
Dk Msolla alisema mchakato huo mabadiliko unasimamiwa na moja ya wadhamini wao GSM baada ya uongozi kuwaomba kutokana na ukweli kwamba gharama zake ni kubwa
GSM imetenga zaidi ya Tsh Bilioni 900 kutekeleza mchakato huo ambao utakuwa ukikamilishwa hatua kwa hatua