Jaffar asubiri mkataba mpya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2020
Jaffar asubiri mkataba mpya Yanga

Mlinzi wa kushoto wa Yanga Jaffar Mohammed anasubiri kusaini mkataba mpya kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Jaffar ni miongoni mwa wachezaji wanaofanya vizuri kwenye kikosi cha kocha Luc Eymael akiwa amebadilishwa majukumu kutoka kiungo wa ushambuliaji na kuwa beki wa kushoto

Jaffar aliyetua Yanga kutoka klabu ya Majimaji, mkataba wake uliongezwa baada ya aliyekuwa kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kupendekeza baada ya Gadiel Michael kutimkia Simba

Awali alitarajiwa kuwa mbadala wa Muharami Issa 'Marcelo' ambaye hata hivyo alishindwa kutamba kupelekea atolewe kwa mkopo klabu ya Singida United

Mwezi Januari Yanga ilimsajili Adeyum Saleh ambaye naye ameshindwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza akimuacha Jaffar akitamba

Katika mchezo dhidi ya Simba uliopigwa March 08 na Bernard Morrison kupeleka kilio Msimbazi, Jaffar alikuwa miongoni mwa nyota wa Yanga waliofanya vizuri

Jaffar amesema kuwa anasubiri kuongeza mkataba kuendelea kukipiga Jangwani

"Mkataba wangu unamalizika mwishoni mwa msimu, yapo mazungumzo ambayo kama yatakwenda vizuri, nitasaini mkataba mpya," amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
10h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
14h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
19h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’