Hawa lazima warudishe heshima ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2020
Hawa lazima warudishe heshima ya Yanga

Mghana Michael Sarpong ameingia kwenye orodha ya wachezaji ambao Yanga inaweza kuwasajili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

Sarpong ni mchezaji huru baada ya klabu ya Rayon Sports kuvunja mkataba wake hivi karibuni pale alipotoa kauli ambayo iliwakera mabosi wa timu hiyo

Huyu Yanga ilijaribu kumsajili mwezi Januari wakati wa dirisha dogo lakini changamoto ya mkataba wake ilitajwa kuwa kikwazo kumnasa

Sarpong alikuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Rwanda msimu uliopita akitupia mabao 16 na msimu huu akiwa ametupia mabao nane kabla ya mkataba wake kuvunjwa

Heritier Makambo yeye anaongoza orodha ya wanaowaniwa na Yanga. Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz alifichua kuwa mabingwa hao wa kihistoria kupitia wadhamini wao GSM, wamemfanya Makambo kuwa chaguo la kwanza katika usajili

Kinachombeba Makambo ni wenyeji wake Yanga licha ya kuwa hakuwa na mwanzo mzuri huko Horoya Ac. Mashabiki wanafahamu uwezo wake kwani alikuwa kinara wa mabao kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria msimu uliopita akifunga mabao 23 kwenye mashindano yote

Hivi karibuni nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi akafichua mpango wa Yanga kumuwania mshambuliaji wa FC Lupopo Mpiana Monzizi ambaye ni kinara wa mabao ligi kuu ya Congo akifungana na Jackson Muleka wote wakiwa na mabao 12

Kupitia mawasiliano ya simu, Monzizi alimhakikishia Tshishimbi kuwa msimu ujao anataka kuja Tanzania kucheza Yanga ambayo ilikuwa imeanza mazungumzo na wakala wake

Winga wa AS Vita Tusila Kisinda nae amedokeza kuwa msimu ujao huenda akacheza soka lake Tanzania kunako klabu ya Yanga. Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Kisinda ameipa kipaumbele Yanga licha ya klabu nyingine kubwa kumuwania

Hivi karibuni kocha mkuu wa Yanga Luc Eymael alidokeza kuwa anahitaji angalau wachezaji saba wapya ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao

Inaelezwa bajeti kubwa zaidi imetengwa kwenye kuimarisha safu ya ushambuliaji ambayo msimu huu imekuwa na mwendo wa kusuasua

Nafasi nyingine ambazo huenda Yanga ikaongeza nguvu ni walinzi wawili (mmoja pembeni mmoja kati) na kiungo mkabaji

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’