GSM yafurahia mauzo ya jezi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2020
GSM yafurahia mauzo ya jezi Yanga

Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM Mhandisi Hersi Said amesema kwa kiasi kikubwa wameridhishwa na mapokezi ya mashabiki wa Yanga katika ununuzi wa jezi za klabu yao

Hersi amesema mwamko huo umewapa hamasa ya kuendelea kufanya kazi na Yanga akiwaahidi Wanayanga kukaa mkao wa kula kwa mapokezi ya jezi mpya kwa ajili ya msimu ujao ambazo zitakuwa bora zaidi kuliko za msimu huu

"Tulitoa matoleo mawili ya jezi yaani Grade A na Grade B. Pamoja na uwepo wa changamoto ya jezi feki,Β  mwamko wa ununuzi wa jezi halisi umekuwa mkubwa sana. Wanayanga wameonyesha kupenda vitu bora kwani hata ukiangalia takwimu za mauzo, zile za Grade A ambao tunaziuza Tsh 35,000/- ndizo zinazonunuliwa zaidi kuliko za Grade B ambazo awali tulikuwa tukiziuza Tsh 25,000/- na sasa tunaziuza Tsh 20,000/- pamoja na nakala ya jarida la klabu ya Yanga," amesema

Aidha Hersi amesema kuelekea msimu ujao wamejipanga kunufaika na mauzo ya jezi za wachezaji wapya ambao watawasajili

"Tunawaambia Wanayanga wakae tayari, kuna usajili mkubwa sana ambao tutaufanya mwaka huu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’