Abdul aunga mkono usajili wa washambuliaji, winga Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2020
Abdul aunga mkono usajili wa washambuliaji, winga Yanga

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul ametoa maoni yake kuhusu aina ya usajili ambao mabosi wake wanapaswa kufanya ili wawe na kikosi bora msimu ujao

Abdul akiwa mmoja wa wachezaji waandamizi Yanga, amesema safu ya ushambuliaji inapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza kwa kusajiliwa nyota wenye uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu

Kinara huyo wa pasi za mabao katika kikosi cha Yanga, amesema kikosi chao chini ya kocha Luc Eymael kinacheza vizuri, wanatengeneza nafasi nyingi lakini changamoto kubwa iliyowakabili ni kushindwa kutumia nafasi hizo kufunga mabao

Abdul pia amedokeza umuhimu wa kuwa na winga ambaye atawatengenezea nafasi washambuliaji bila ya kusahau nafasi ya mlinzi wa kushoto kwa kuwa wanamtegemea zaidi Jaffar Mohammed

Licha ya kumsajili Adeyum Saleh dirisha dogo, nyota huyo anakabiliwa na majeraha ya mara kwa mara lakini pia ameshindwa kufikia matarajio

Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amedokeza kuwa wanatarajia kusajili wachezaji saba wapya

Safu ya ushambuliaji inatarajiwa kuwa na maingizo mpya huku jina la mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Heritier Makambo likiwa miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa mbioni kurejea Jangwani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’