Beki wa kushoto wa Yanga Adeyum Saleh amesema pamoja na ligi kusimama kutokana na janga la corona, wanaendelea kufanya mazoezi kikamilifu ili kuhakikisha wanakuwa fiti pale ligi itakaporejea
Adeyum alirejea visiwani Zanzibar ambako aliungana na nyota wengine wa Yanga Feisal Salum na Abdulaziz Makame kujifua pamoja
Mwamba huyo aliyetua Yanga usajili wa dirisha dogo, amesema wanajiweka timamu ili waipambanie na kurejesha heshima ya Yanga
"Tunafanya mazoezi ili kujiandaa na ligi. Tuko vizuri tunajifua majumbani tukitekeleza maelekezo tuliyopewa na walimu wetu. Tupo tayari kuipambania Yanga ili turudishe nafasi na heshima yetu katika soka la Tanzania," amesema
Adeyum alianza vyema maisha yake kunako kikosi cha Yanga aliposajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria mwezi Januari
Hata hivyo majeraha ya mara kwa mara yamemfanya ajikute kwenye ushindani mkali kutoka kwa kiraka Jaffar Mohammed ambaye kwa siku za karibuni anaonekana kuaminiwa zaidi ya kocha Luc Eymael