Mwakalebela ataja mafanikio mwaka mmoja wa uongozi wao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2020
Mwakalebela ataja mafanikio mwaka mmoja wa uongozi wao

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Fredrick Mwakalebela amesema Amani na Utulivu unaoonekana kwenye klabu ya Yanga sasa ni moja ya mafanikio wanayojivunia katika uongozi wao ambao umetimiza mwaka mmoja

Mwakalebela amesema ni muhimu kwa klabu kuwa na utulivu kabla ya kufikiria mambo makubwa

"Kama unavyofahamu, tangu tumeingia madarakani, timu imekuwa na utulivu. Ni hatua muhimu katika kutekeleza malengo tuliyojiwekea. Kwani hakuna jambo lolote linaweza kufanyika pasi na kuwepo Amani na utulivu," amesema

"Lakini pia tumeweza kuunda kikosi cha ushindani ambacho sasa kinashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakati huu ligi ikiwa imesimama kutokana na janga la corona"

"Pia tuko hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), hii ni ishara kuwa timu yetu iko katika njia sahihi"

Mwakalebela pia amekumbushia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani zao Simba March 08

Suala la mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya Yanga ni jambo jingine ambalo Mwakalebela aliligusia

"Tutafanya kazi na wataalam kutoka Hispania ambao watatupa njia sahihi ya kufuata ili kufanikisha kubadili klabu yetu na hili ni jambo ambali kila Mwanayanga anaweza kujivunia"

Mwakalebela amebainisha kuwa kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa kudhibiti matumizi yasiyo halali ya nembo la klabu ya Yanga, wameingia mkataba na GSM ambao wanasimamia usambazaji wa jezi na bidhaa nyingine zenye nembo ya klabu hiyo

Kuzindua Jarida, website na App ni mafanikio mengine ambayo Mwakalebela amesema wanayanga wanajivunia

Mwakalebela amesem changamoto zilizopo ni pamoja na suala la jezi feki kwani pamoja na hatua muhimu zinazochukuliwa, bado wapo watu wachache wasio waaminifu wanawarudisha nyuma

Lakini pia amezungumzia tabia ya baadhi ya wadau miongoni mwao kutumia vyombo vya habari vibaya kwa kuchafua taswira ya klabu ya Yanga kwa amaslahi yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’