Mkandala atajwa kumalizana na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 May 2020
Mkandala atajwa kumalizana na Yanga

Inaelezwa klabu ya Yanga iko mbioni kumalizana na kiungo fundi wa Tanzania Prisons Cleofas Mkandala

Nyota huyo ambaye tetesi zilimuhusisha kuwaniwa na Azam Fc, mambo yakiwa sawa huenda msimu ujao akavaa uzi wa njano na kijani

Mtu wa karibu wa kiungo huyo amedokeza uwepo wa mazungumzo kati yake na Yanga huku akibainisha usajili wake huenda ukakamilishwa punde tu dirisha la usajili litakapofunguliwa

Yanga ilijaribu kumsajili Mkandala usajili wa dirisha dogo akiwa miongoni mwa wachezaji waliokuwa wamependekezwa na kocha Charles Mkwasa wakati ule

Mkandala ameng'ara kwenye kikosi cha Prisons msimu huu, akiwa mmoja wa wachezaji waliokuwa wameitwa na kocha Etienne Ndayiragije kuunda kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani

Hata hivyo michuano hiyo imepigwa kalenda mpaka mwakani kutokana na janga la corona

Ukizungumzia wachezaji mafundi kwenye ligi kuu ya Vodacom, huwezi kukosa kutaja jina la Mkandala

Kiungo huyu mwenye umri wa miaka 21, anamudu vyema kucheza namba nane pamoja na nafasi zote za pembeni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’