Ni utaratibu gani utumike kumaliza msimu VPL?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2020
Ni utaratibu gani utumike kumaliza msimu VPL?

Suala la ligi kuejea limeshabainishwa na Rais wa nchi Dk John Magufuli, kinachosubiriwa ni Serikali kutoa ruhusa baada ya kujiridhisha na mwenendo wa ugonjwa wa corona nchini

Lakini pia imeelezwa ligi itakaporejea mashabiki hawataruhusiwa kuingia viwanja, kwa maana mechi zote 90 zilizobaki zitachezwa bila ya mashabiki

Mjadala uliopo ni kuhusu utaratibu gani utumike kukamilisha mechi zilizobaki kutokana na mazingira yaliyopo

Ipo hoja kuwa timu nyingi zimeathirika kiuchumi kutokana na janga la corona hivyo utaratibu wa mechi kupigwa nyumbani na ugenini huenda ukasababisha changamoto zaidi kwa timu

Hapa pia suala la mechi kupigwa bila ya mashabiki na wakati timu nyingi hutegemea zaidi mapato ya milangoni, linaongeza hofu kwa vilabu kuwa huenda vikashindwa kumudu gharama kama ikitokea havitapewa msaada wa kifedha

Hivyo yapo mapendekezo ya baadhi ya wadau waliowengi ambao wanadhani ni vyema ligi ikachezwa katika kanda au kuchagua viwanja vichache ambavyo mechi zote zitapigwa

Mfumo huu unaweza pia kusaidia udhibiti wa wahusika wa timu zote kwani ikumbukwe kutakuwa na vipimo vya corona kabla ya mchezo wowote kuruhusiwa kupigwa

Lakini wapo wanaodhani utaratibu wa kawaida uendelee kutumika. Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting Massau Bwire alikwenda mbali zaidi kwa kusema ni bora ligi ikafutwa kama kutakuwa na ulazima wa kubadili mfumo wa kucheza mechi zilizobaki

Amesema kila timu inastahili kupewa haki yake, kubadili utaratibu wa mechi wakati huu utazinyima haki baadhi ya timu ambazo hazitakuwa na nafasi ya kutumia viwanja vyao vya nyumbani

Je tunamaliza vipi ligi?

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’